WANANCHI WAPATA TAHARUKI HOFU YATANDA, MAMLAKA YAFAFANUA LILIKUA ZOEZI UOKOAJI

WANANCHI WAPATA TAHARUKI HOFU YATANDA, MAMLAKA YAFAFANUA LILIKUA ZOEZI UOKOAJI

Meneja wa Viwanja vya Ndege Kanda ya Magharibi, Fadhili Magehema amesema zoezi la uokoaji na utayari wa kukabiliana na ajali za ndege lililofanyika leo Mei 13 limefanyika kufuatia agizo la mamlaka ya anga linalotaka zoezi hilo kufanyika angalau mara moja kila baada ya miaka miwili, kwa lengo la kuongeza uwezo wa kukabiliana na majanga ya ndege kwa haraka na ufanisi.

Akiizungumza wakati wa zoezi hilo, amesema zoezi Hilo limehusisha vikosi mbalimbali vya uokoaji, zimamoto, wahudumu wa afya pamoja na mamlaka za usalama ili kuongeza ufanisi wa utoaji huduma za haraka katika matukio ya dharura viwanjani.

Kutokana na taharuki iliyojitokeza kwa baadhi ya wananchi waliohisi huenda kulikuwa na ajali halisi ya ndege, vyombo vya usalama vimelazimika kutoa ufafanuzi na kuwataka wananchi kuondoa hofu, huku vikisisitiza kuwa tukio hilo lilikuwa ni zoezi maalum la mafunzo ya kiutayari.

Zoezi hilo limefanyika katika Kiwanja cha Ndege cha Mkoa wa Katavi kwa kushirikisha wadau mbalimbali wa huduma za dharura na usalama.