TWAHA KIDUKU ATUA KATAVI KUSHUHUDIA PAMBANO LA NGUMI

TWAHA KIDUKU ATUA KATAVI KUSHUHUDIA PAMBANO LA NGUMI

Bondia maarufu nchini, Twaha Kiduku, amewasili mkoani Katavi kushuhudia pambano la ngumi litakalowakutanisha mabondia mbalimbali, huku pambano kuu likimkutanisha Jafari Chingwaba, maarufu kama J Fighter, wa Katavi dhidi ya Habibu Pengo wa Dar es Salaam.


Mapambano hayo yanalenga kutafuta vipaji vipya, kukuza vipaji vilivyopo na kuinua mchezo wa ngumi nchini, huku ujio wa Twaha Kiduku ukiwa sehemu ya kuvutia wadau na mashabiki wa mchezo huo.