HIFADHI YA KATAVI NDIO PORI HALISI LA AFRICA

HIFADHI YA KATAVI NDIO PORI HALISI LA AFRICA

HIFADHI YA TAIFA KATAVI:Hifadhi ya Taifa ya Katavi ni moja ya hifadhi kubwa na za kipekee nchini Tanzania, iliyopo mkoani Katavi, magharibi mwa nchi. Hifadhi hii ilisimamiwa na kuanzishwa rasmi mwaka 1974 na inasimamiwa na Tanzania National Parks Authority (TANAPA).

Ina ukubwa wa takribani kilometa za mraba 4,471 na ni miongoni mwa hifadhi tano kubwa nchini. Katavi inajulikana kwa wanyamapori wengi katika mazingira asilia yasiyo na msongamano wa watalii. Inahifadhi makundi makubwa ya nyati, tembo, viboko na mamba, hasa katika mabonde ya mito ya Katuma na maziwa ya msimu kama Chada na Katavi.

Kwa upekee wake wa ukimya wa pori halisi (untouched wilderness), Katavi ni kivutio muhimu cha utalii wa picha na utafiti wa wanyamapori, na ina mchango mkubwa katika uchumi wa utalii wa Tanzania.