RAIS SAMIA KUWATUNUKU TUZO WALIPA KODI BORA

RAIS SAMIA KUWATUNUKU TUZO WALIPA KODI BORA

Rais Samia Suluhu Hassan, anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika hafla ya utoaji wa tuzo za mlipakodi bora zitakazotolewa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Julai 1, 2026 katika ukumbi wa Mlimani City.

Tuzo hizo zinalenga kuwatambua na kuwapongeza walipakodi waliotekeleza wajibu wao kwa uaminifu, huku zikihamasisha utamaduni wa ulipaji kodi kwa hiari na kwa wakati nchini.

Sambamba na hafla hiyo, TRA itaadhimisha miaka 30 tangu kuanzishwa kwake mwaka 1996, katika sherehe zitakazolenga kuenzi mchango wa walipakodi katika maendeleo ya taifa.

Maadhimisho hayo yanatarajiwa kuwakutanisha viongozi mbalimbali wa serikali, sekta binafsi na wadau wa maendeleo.