KATIBU MKUU DKT. MAGEMBE ASHIRIKI MKUTANO WA ReSCO

KATIBU MKUU DKT. MAGEMBE ASHIRIKI MKUTANO WA ReSCO

Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Dkt. Grace Magembe akishiriki Mkutano wa Nne wa Kamati ya Uongozi ya Ukanda wa Afrika wa Mawaziri wa Afya (ReSCO), unaofanyika leo tarehe 18 - 19 Agosti 2026 jijini Dar es Salaam.

Dkt. Magembe anaungana na Mawaziri kutoka nchi 14 za Afrika katika mkutano huo unaojadili ajenda muhimu za afya, ikiwemo afya ya uzazi, mama, mtoto na vijana pamoja na kuimarisha mifumo ya kukabiliana na magonjwa ya mlipuko.

Mkutano huo umeandaliwa kufuatia kikao cha Kamati ya Wataalamu wa Afya ya Kikanda (ReTAC) kilichoongozwa jana na Dkt. Magembe jijini Dar es Salaam, ambapo wataalamu walipitia na kuunganisha mapendekezo ya kitaalamu yatakayowasilishwa katika Mkutano huu wa ReSCO.