DKT.MWIGULU: SERIKALI KUONGEZA KASI YA UJENZI WA  BARABARA YA KAREMA

DKT.MWIGULU: SERIKALI KUONGEZA KASI YA UJENZI WA BARABARA YA KAREMA

Mnamo tarehe 13 mwezi wa Machi mwaka 2026 Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Mwigulu Nchemba alifanya ziara ya kikazi Mkoani Katavi ambapo pamoja na Mambo mengine aliweka jiwe la Msingi Ujenzi wa Barabara ya Mpanda Karema yenye urefu wa Kilomita 112.

Katika sehemu ya Hotuba yake Waziri Mkuu aligusia jitihada zilizowekwa na Serikali za kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo Nchini ikiwemo barabara hii.

Barabara hii ambayo kwa sasa ujenzi wake umefikia zaidi ya asilimia 40 ,si tuu kwamba itawanufaisha wafanyabiashara ambao wanaitumia Bandari ya Karema laasha ,bali hata wananchi wanaoishi pembezoni mwa barabara hiyo.