DKT. KIJAJI AIPA BODI YA TWPF MAELEKEZO MAZITO YA UHIFADHI NA UWEKEZAJI

DKT. KIJAJI AIPA BODI YA TWPF MAELEKEZO MAZITO YA UHIFADHI NA UWEKEZAJI

Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Ashatu Kijaji, ameielekeza Bodi ya Wadhamini ya Mfuko wa Kuhifadhi Wanyamapori Tanzania (TWPF) kuweka kipaumbele katika kutafuta suluhisho la migongano kati ya binadamu na wanyamapori wakali na waharibifu ili kulinda maisha na mali za wananchi wanaoishi karibu na maeneo ya uhifadhi.

Akizungumza jijini Dodoma wakati wa kikao na bodi hiyo iliyoongozwa na Jafari Kideghesho, Dkt. Kijaji pia alisisitiza umuhimu wa uwekezaji wenye kuongeza vyanzo vya mapato vya mfuko, ikiwemo miradi ya ukumbi wa kisasa wa mikutano na hoteli.


Kwa upande wake, Prof. Kideghesho amesema bodi itatekeleza maelekezo hayo kwa lengo la kuimarisha uhifadhi, kufanya tafiti na kupunguza changamoto za wanyamapori wakali na waharibifu kwa manufaa ya wananchi.