CCM KATAVI YAWANOA MAKADA ZAIDI YA 5,000, ILEMBO YATAKA MAFUNZO ENDELEVU

CCM KATAVI YAWANOA MAKADA ZAIDI YA 5,000, ILEMBO YATAKA MAFUNZO ENDELEVU

 

Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Katavi kimeendelea kuwajengea uwezo viongozi na makada wake kupitia mafunzo ya itikadi, yakilenga kuimarisha uelewa wa misingi na maadili ya chama pamoja na kujenga uwezo wa kutekeleza majukumu yao ya kichama.

 

Mafunzo hayo yaliyoanza Oktoba 9, 2026, yamehusisha zaidi ya makada 5,000, yakishirikisha viongozi mbalimbali, akiwemo Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Katavi, Ndugu Iddi Kimanta, Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya ccm taifa mkoa wa katavi MNEC Ndugu Gilbert Sampa na Katibu wa CCM Mkoa wa Katavi, Ndugu Hawa Siri Makonyola pamoja na viongozi mbalimbali.

 

Na oktoba 18 Mafunzo hayo yaliyohitimishwa kwa  Kata ya Ilembo, yakiwa sehemu ya juhudi za kuimarisha uelewa wa viongozi na makada kuhusu misingi ya chama na kujenga imani ya CCM kwa wanachama na wananchi katika mazingira ya siasa za ushindani.

 

Katika hitimisho hilo washiriki wa Kata ya Ilembo wameomba mafunzo hayo yawe endelevu na yatolewe mara kwa mara ili kuwapa fursa ya kuongeza maarifa na kuimarisha uwezo wao katika kutekeleza majukumu ya kichama.

 

CCM Mkoa wa Katavi inaendelea kuweka mkazo katika kuwajengea uwezo viongozi na makada wake, hatua inayolenga kuimarisha chama kuanzia ngazi ya chini na kuhakikisha misingi na maadili yake vinaendelea kuzingatiwa katika utekelezaji wa majukumu ya kichama.