AGIZO LA WAZIRI MKUU DKT. MWIGULU KATAVI WALIMU WA KUJITOLEA WASHANGILIA

AGIZO LA WAZIRI MKUU DKT. MWIGULU KATAVI WALIMU WA KUJITOLEA WASHANGILIA

 Agizo la Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa,Dkt. Mwigulu Nchemba la kupiga marufuku wazazi kuchangishwa hela za kuwalipa walimu wa kujitolea limetekelezwa kwa Kishindo na UONGOZI wa Serikali ya mkoa wa katavi

Awali wazazi walikuwa wakijichangisha Fedha ili kuwalipa Walimu Wawili wa kujitolea Kwenye shule ya msingi ya KIBAONI Halmashauri ya Mpimbwe wilaya ya Mlele shilingi laki mbili kila Mwezi jambo lililokuwa likiwakera na kulazimika kutoa kilio chao kwa Waziri mkuu wakati wa Zoezi la kusikiliza na kutatua kero za wananchi Kwenye wilaya ya mlele

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mpimbwe Shamimu Mwariko amesema kuwa siku ileile mara baada ya maagizo ya Waziri Mkuu alichukua hatua ya usitishwaji wa Michango hiyo na sasa Halmashauri inawalipa walimu kupitia mapato ya Ndani.